Msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kuelezea Jinsi ugonjwa Wake ulivyotaka kumuua Wiki chache zilizopita.
Katika mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Ommy DImpoz amefunguka kuhusu ugonjwa wake wa koo ulivyokuwa ukimsumbua na kusema alibakiza wiki moja tu angefariki dunia kwani madhara ya tatizo alilokuwa nalo yalikuwa makubwa na sumu ilikaribia kuingia kwenye maini.
Wakati sijafanyiwa upasuaji wa kwanza, madaktari waliniambia upasuaji utakuwa mkubwa, hivyo wakanikupa muda wa kukaa na kujitafakari tena na nikaongea na familia yangu pamoja na wasimamizi wangu na wao waliniambia tunaimani kuwa nitatoka salama na kunisihi kufanya upasuaji na nikafanya.
Upasuaji ulichukua saa sita mpaka kumi na moja. Madaktari walikata tumboni mpaka karibia na kifua, pia shingoni na sehemu zingine na walifanya hivyo ili kupandisha tumbo juu na vitu vingine ili kuhakikisha wananusuru maisha yangu.
Nilivyoenda Ujerumani, walivyonicheki wakagundua ‘usaha’ umezidi na unakaribia kuingia kwenye maini na nilibakiza wiki moja tu, ningechelewa basi habari ingekuwa imeisha. Walinifanyia upasuaji wa dharula na waliniambia ingechukua saa nne lakini ilichukua saa 8, nilikaa hospital wiki tatu, nashukuru imenisaidia na kwa sasa naendelea vizuri Alhamdulillah“. Hivi sasa Ommy Dimpoz ambaye amerejea nchini siku chache zilizopita ameonekana kuendelea vizuri na hata kutoa wimbo wake mpya.

Comments
Post a Comment