Baada ya kuanzisha biashara yake ya duka la nguo za watoto liitwalo 'Little Sweetheart', staa wa kike wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu amepewa masharti na familia yake namna ya kuliendesha duka hilo, pamoja na kuachana na baadhi ya marafiki wasiokuwa na faida kwake.
Moja ya chanzo chetu cha kuamini kimesema kuwa "Nuru ndiye anayesimamia kila kitu dukani hapo kuliko kumwachia Wema mwenyewe ambae wanamjua ana mambo mengi hivyo usimamizi unaweza kumshinda na hata huyo Wema mwenyewe lazima afuate maelekezo ya Nuru kwani hata habari za kuzunngumza na media pia amekatazwa Nuru ndie atakuwa anazungumza kwa niaba yake kwa sasa hivi"
Itakumbukwa kwamba Duka hilo la Wema lililopo Kinondoni jijini Dar es salaam, ni la pili baada ya lile la kwanza lililomshinda, ambalo lilikuwa likiuza lipstick zake za 'Kiss by Wema' lililokuwa maeneo ya Mwenge, jijini Dar es Salaama na kutajwa chanzo cha kumshinda ni marafiki hivyo sasa hivi familia inamchagulia baadhi ya marafiki kuwa nao.
TOA MAONI YAKO HAPA

Comments
Post a Comment