MOSE IYOBO AWACHANA WANAOIBEZA KAZI YAKE

Mose Iyobo amesema yeye elimu yake ni darasa la saba na anawashangaa baadhi ya watu wanaoibeza kazi yake ya kuwa back up dancer wa Diamond. Amesema wanaombeza wengine elfu 10,000 kwa siku wanaipangia bajeti ya chakula cha siku nzima au zaidi wakati yeye buku 10 hiyo kwa siku huitumia kununua vocha ya simu kwa ajili ya kuongea tu na mwanae Cookie. Amewataka watu wasidharau kazi za wengine ambapo za Kwao hazina faida kwa wanaowadharau
.
Kuhusu alikutanaje na Diamond hadi kuanza kufanya nae kazi, Mose ameiambia GPL kuwa alisoma shule moja ya msingi na Diamond isipokuwa Mond alikuwa amemtangulia madarasa mawili. .
.
Amesema kuna siku wote walienda kwenye show flani ya kusaka vipaji chipukizi ambapo Diamond alienda kuonesha kipaji chake cha kuimba na yeye alienda Kama dancer na baada ya kuonana hapo kwa kuwa walisoma shule moja Diamond alimuomba Iyobo waungane waendelee kupambana hadi kieleweke watoke kimaisha na wao kupitia muziki
.
Iyobo anakiri kuwa hakuna changamoto yoyote ya kufanya kazi na Diamond isipokuwa yeye anapokuwa kwenye mishe zake mwenyewe watu wengi humfata wakijua yupo na Mond na kumuuliza superstar huyo yuko wapi
.
Dancers wa WCB wote wanatajwa kila mmoja ashajenga nyumba yake na kufungua biashara nzuri huku wakiendelea na kudance. Iyobo anasema licha ya kuwa hajasoma hata secondary anafurahi kuwa na maisha mazuri na kutembelea nchi nyingi kupitia kipaji chake hicho huku akisema amechangia pia kuwa-inspire baadhi ya vijana wenzie waivhukulie serious kazi ya back up dancers Kama zilivyo kazi nyingine .
.
Anasema anajua hawezi kuwa dancer miaka yake yote so anawekeza pia maeneo mbalimbali. Kwasasa ni choreographer pia wa kazi mbalimbali na amesema Diamond hajawahi kumzuia kufanya kazi na mtu mwingine so anayemhitaji no suala la makubaliano tu ya kibiashara kupitia mikataba
.
Fun fact: Mose Iyobo anatajwa kuwa dancer wa kwanza Tanzania kutajwa kuwania tuzo nyingi nje ya nchi kuliko dancer yeyote Yule.
TOA MAONI YAKO HAPA

Comments