MAMA DIAMOND AFUNGUKA UKARIBU WA OMMY DIMPOZ NA ZARI

MAMA wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ a.k.a Mama D ameufungukia ukaribu wa mkwewe Zarinah Hassan ‘Zari’ na mwanamuziki Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuwa ni wa kawaida na yeye anaona ni fresh tu.  Mama D aliliambia Risasi Jumamosi kuwa ukaribu wa Zari na Dimpoz ni wa kawaida kama watu wengine na kuwataka watu waache manenomaneno yasiyo na msingi. “Kwani kuna ubaya gani? Hivyo ni vitu vya kawaida kwa mtu kukumbatiana na mtu aliyekutana naye,” alisema Mama D.Alipoulizwa kuhusu Dimpoz kufikia hatua ya kupapasa paja la Zari, mama huyo alisema kuwa hajaona picha hiyo ila akazidi kusisitiza kuwa, haoni tatizo lolote kwani huenda wamekutana na kuongea kama watu wengine.
Image result for zari na ommy dimpoz
“Mimi sijaona hiyo picha ambayo kamshika pajani lakini bado nasema hayo ni mambo ya kawaida tu. Ina maana Zari asiongee na watu? Watu wanasema Nasibu na Ommy wana ugomvi, mimi sijaona wakipigana, najua wanaongea na wala mimi sina ugomvi na mtu,” alisema Mama D.


Comments